News

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

PRECISION AIR YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA TANO

Dar es Salaam. Novemba 8 2019... Shirika pekee la ndege Tanzania lililo orodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam, Precision Air Services plc, limefanya mkutano wake mkuu wa tano wa wanahisa washirika hilo.Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw.Michaell Shirima, ulijadili taarifa ya fedha kwa mwaka 2017/18.

Katika kikao hicho wanahisa walitaarifiwa kuwa kwa mwaka 2017/2018, shirika la Precision Air liliingiza faida kabla ya makato kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 1.4 kwa mwaka ulioisha Machi 31 2018. Akizungumza na wanahisa katika mkutano, bwana Michael Shirima alisema, sekta ya usafiri wa anga imepita katika vipindi mbali mbali ambavyo vilipelekea mabadiliko ya uelekeo wa soko.

“Tumeshuhudia ongezeko la ushindani kwenye soko lakini licha ya hayo tumendelea kufanya vizuri katika utendaji kazi wetu kwani tumekua tukishuhudia kupungua kwa hasara mwaka hadi mwaka. Tunajiamini kuwa kwa mpango mkakati wa kibiashara uliopo, katika miaka miwili ijayo tutaweza kutengeneza faida.” Alisema.

Kwa upande mwingine, Bw.Shirima alitoa taarifa ya kuongezeka kwa mapato kwa 43% katika mwaka 2017-2018 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2016-2017 ambayo pia yameongezeka kwa asilimia 7 kulinganisha na mwaka 2015-2016.
“Katika mtandao mzima, jumla ya abiria waliosafirishwa ilikuwa 474,247 ikiwa ni ongezeko la 16% ikilinganishwa na abiria 408,807 waliosafirishwa katika mwaka wa fedha 2016/17.” Aliongeza.

Akidokeza juu ya mipango ya shirika hilo, Bw.Shirima amesema kuwa kampuni itatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano ambao unatarajiwa kugeuza hasara ya Shilingi za Kitanzania bilioni 21 kabla ya kodi, kuwa faida. Amefafanua kuwa hasara hiyo imechangiwa na mlimbikizo wa gharama za umiliki wa ndege na kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani.

“Tunaridhishwa na utendaji wetu kwani, tumeendelea kushuhudia kupungua kwa hasara mwaka hadi mwaka, hii ikiwa ni isharia kuwa tupo katika njia sahihi katika mkakati wetu wa kutengeneza faida katika biashara. Kwa mwaka 2017-2018 hasara ilipungua kwa 28% ikilinganishwa na mwaka 2016-2017 na 69% ikilinganishwa na mwaka 2015-2016,” Alieleza Bw.Michael.

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa shirika la ndege la Precision Air, Bw.Patrick Mwanri, alisema kwamba Precision Air itajidhatiti katika uboreshaji wa ufanisi, kupunguza la gharama za uendeshaji na matumizi, matumizi bora ya ndege yenye kuleta tija, kuimarisha ushirikiano na washirika na kuongeza vyanzo vya ziada vya mapato kama mkakati wa kuleta mapinduzi katika biashara ndani ya miaka mitano ijayo.

“Tunatazamia kupata faida kufikia mwaka 202, hii ikiwa ni matokea ya utekelezwaji kamilifu na wa mafaniko wa mpango makakati wetu wa mitano. Pia tunatarajia kufikia malengo haya kwa kutoa huduma bora zitakazo kidhi matarajio ya wateja wetu,” Aliongeza.

Kuhusu Shirika la Ndege la Precision Air

Precision Air ni shirika la umma lililoanzishwa mnamo mwaka 1993 na linatoa huduma za usafiri wa anga kwenda sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Safari zake huanzia makao yake yaliyoko makuu Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Serengeti, Mtwara, Kahama, Bukoba, Mwanza, Zanzibar, Tabora, Serengeti, Nairobi, Entebbe na makao makuu ya nchi Dodoma. Huduma nyingine zinazotolewa na shirika ni pamoja na huduma za ubebaji mizigo kwa njia ya anga. Hali kadhalika shirika la Precision Air limewahi kupokea tuzo kadha wa kadha kutoka Tanzania Society of Travel Agents, Africa Aviation News Port, Tanzania Leadership Awards, TASOTA, na pia kampuni ni mshirika wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.

We are using cookies to personalize and enhance your use of the Precision Air Website. By continuing to use our website without changing your cookie settings, you are agreeing to the use of cookies as set in the Precision Air Privacy Policy.